Habari za Punde

WAZE WASIOJIWEZA WAPEWA MSAADA PEMBA

Na Abdi Suleiman, Pemba

WIZARA ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Pemba, imekabidhi msaada kwa wazee wanaoishi katika nyumba ya wazee wenye thamani zaidi ya shilingi 600,000 kwa ajili ya sikukuu ya Eid el Fitri.


Akikabidhi msaada huo, Ofisa Mdhamini wa wizara hiyo Pemba, Maua Makame Rajab, alisema lengo la kutoa msaada huo ni kuwaenzi na kuwatunza wazee ili wajione binaadamu wengine wanaostahiki kusherekea vyema siku hiyo.

Hayo aliyasema huko Limbani, Wete Pemba, katika nyumba ya Idara ya Ustawi wa Jamii ambako wazee wasiojiweza hutunzwa, wakati wa kukabidhi msaada wa vitu mbali mbali kwa wazee hao.

Ofisa huyo, alifahamisha kuwa, ipo haja kwa watu mbali mbali na wafadhili kujitokeza kwa wingi kuweza kuwapatia wazee misaada na wao kujiona ni sehemu ya jamii kutokana na kuwa na mahitaji mbali mbali.

Msaada waliopatiwa ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, sukari, tambi, viatu, nguo, sabuni, na nyama, nyumba ya wazee Wete ina jumla ya wazee wanane ambapo wanaume saba na mwanamke mmoja.

Aliwataka wazee hao kuvitua vitu walivyokabidhiwa na kuacha kwenda kuviuza kwa watu wengine kwani kufanya hivyo lengo litakuwa halijafanikiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.