Habari za Punde

WAISLAMU WAKITHIRISHE SADAKA WAKATI WA EID

Na Bakari Mussa, Pemba

WAISLAMU wametakiwa kuitumia sikukuu ya Eid el Fitri kwa kupeana sadaka kwa wale wenye uwezo ili kuwafanya waislamu wasio na uwezo nao kupata fursa ya kuisherekea siku hiyo kwa furaha kubwa jambo ambalo litaimarisha udugu miongoni mwao.


Hayo yameelezwa na Sheikh, Ali Suleiman, wakati akitoa hutuba ya swala ya Eid el Fitri iliyosaliwa katika msikiti wa Qadiria, uliopo Wawi Chake Chake Pemba.

Alieleza kuwa waislamu wenye uwezo ni wajibu wao kuwasaidia wale wasio na uwezo ili kujenga mapenzi mema hasa ikizingatiwa kuwa waislamu ni ndugu baina yao.

Khatib huyo, aliwataka waislamu kuwa makini kwa kuisherekea sikuku hiyo kwa misingi ya dini yao inavyoelekeza ili wasiingie katika makosa makubwa sambamba na kuzidisha ibada kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu.

Alifahamisha kuwa kumalizika kwa mwezi wa Ramadhani hakumanishi kumalizika kwa ibada, kwani Mwenyezi Mungu ambaye ndiye anayeabudiwa yupo.

Alisema kufanya zinaa siku ya Eid ni sawa na kufanya hivyo siku ya kiama, hivyo aliwasisitiza waislamu kuzinasihi nyoyo zao na jambo hilo.

Naye Haji Nassor, kutoka Chambani anaripoti kuwa waislamu wametakiwa kuwavalisha watotowao mavazi ya kiislamu watoto wao kwani kuwafanya hivyo watakuwa katika maadili mema ya Kiislamu.

Imamu wa msikiti wa Chumbagani Wambaa- Pemba, Haji Hamad Ussi, alieleza hayo kwenye hotuba ya swala ya Eid iliyohudhuriwa na waislamu wa eneo hilo.

Aliwataka wazazi wa kiislamu na familia zao kusherehekea siku hiyo kwa madili ya kiislamu kwani kufanya hivyo ni kuwajengea wema kwa Allah.

Aidha aliwasihi kushikama pamoja katika dini jambo ambalo litazidisha uimara wa dini hiyo, pamoja na kuwa ni mara moja kwa mwaka kufikiwa na mwezi wa Ramadhani, lakini waufanye kama ni darasa kwao kwa kuyaendeleza yale yote waliokuwa wakiyafanya katika mwezi huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.