Yanga yamzawadia Manji
L Yatwaa ubingwa Kagame mgongoni mwa Azam
Na Mwandishi Wetu
MABAO mawili yaliyofungwa kila kipindi, jana
yaliiwezesha Yanga kulibakisha
kombe la Kagame kwa mwaka wa pili mfululizo.
Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Azam FC, katika mchezo wa fainali uliokuwa mkali na wa kuvutia katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu hizo ziliuanza mchezo kwa utulivu huku
kila upande ukiusoma mwengine, lakini Azam ilianza kwa kutawala zaidi sehemu ya
katikati wakati wa kipindi cha kwanza.
Mshambuliaii matata wa Azam John Bocco,
hakuweza kuonesha makeke yake kwani aliwekwa chini ya ulinzi wa kipolisi na
Kevin Yondani, aliyemnyima nafasi ya kufurukuta, ingawa mara kadhaa alijaribu
kuponyoka bila mafanikio.
Hata hivyo, kadiri muda ulivyokwenda, ndivyo
wachzeaji wa timu hz walipwea kujikunua na kshambulaakwa zamu, ingawa milango
iliendelea kuwa migumu kufunguka.
Wakati muamuzi akijiandaa kupuliza firimbi
kuashiria mapumziko, mchezaji Hamisi Kiiza aliwainua mashabiki wa Yanga kwa
kuandika bao mnamo dakika ya nyongeza ya kipindi cha kwanza, baada ya kumzidi
ujanja mlinzi Aggrey Morris aliyekuwa amemsahau Mganda huyo.
Miamba hiyo ilikianza kipindi cha pili kwa si
huku Azam ikibadilika na kuliandama lango la Yanga lakini kikwazo kikubwa
kilikuwa golikipa Ali Mustafa ambaye mara kwa mara alilazimika kufanya kazi ya
ziada kuokoa michomo ya Ibrahim Mwaipopo, John Bocco na Mrisho Ngassa
aliyeingia kipindi cha pili.
Mshambuliaji mahiri Saidi Bahanuzi,
aliihakikishia Yanga ubingwa baada ya kuifungia bao katika dakika ya pili ya
mwamuzi Thierry Nkurunzinza kutoka Burundi, baada ya kuwakimbia kwa kasi
walinzi wa Azam na kuachia shuti la nguvu lililokwenda moja kwa moja nyavuni.
Nayo AS Vita Club kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, imefanikiwa kuramba dola elfu kumi kwa kushika nafasi ya
tatu baada ya kuichapa APR ya Rwanda kwa mabao 2-1.
Mabao ya washindi katika mchezo huo, yalifungwa
na Magola Mapanda katika dakika ya 18 na Mutombo Kazadi dakika ya 67, huku
maafande wa APR, wakifungiwa na Jean Mugiraneza mnamo dakika ya 89.
Kwa ushindi huo, Yanga imetia mfukoni dola elfu
30 na Azam dola 20,000, ambazo zimetolewa na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
No comments:
Post a Comment