Habari za Punde

Waandishi Wazuru Sehemu za Kihistoria


Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali walifika huko Mangapwani na kupata historia ya Kisima cha chini kwa chini kwa Mkuu wa huduma za Elimu Makumbusho Mwalimu Ramadhan Ali

Hichi ndio kisima cha Chini kwa chini kilichokuwepo huko Mangapwani Mkoa wa kaskazini Unguja.
Waandishi wa Habari wakiwa Ndani ya Kisima cha Chini kwa chini chenye Urefu wa zaidi ya Kilomita moja katika kila pembe ya ndani ya kisima hicho

Wanahabari wakiingia ndani ya Handaki lililojengwa na Utawala wa Kikoloni kwa ajili ya kujilinda na Vita Mwaka 1939-1945

Hili ndilo handaki lililojengwa na Utawala wa Kikoloni kama linavyoonekana kwa ndani

Hii ni nyumba ya chini kwa chini iliojengwa na Waarabu kwa ajili ya maficho ya Watumwa baada ya kupigwa marufuku Biashara hio mwaka 1873 huko katika kijiji cha Mangapwani kaskazini Unguja.

Mkuu wa huduma za Elimu Makumbusho Mwalimu Ramadhan Ali akiwaongoza Waandishi kuingia ndani ya Nyumba ya chini kwa chini iliojengwa na Waarabu kwa ajili ya maficho ya Watumwa baada ya kupigwa marufuku Biashara hio mwaka 1873 huko katika kijiji cha Mangapwani kaskazini Unguja.

 PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.