Habari za Punde

CHANEZA kuchaguana Sept 8


Na Mwajuma Juma
UCHAGUZI mkuu wa Chama cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA), unatarajiwa kufanyika Septemba 8 mwaka huu.

Katibu wa kamati inayosimamia uchaguzi huo Kibabu Haji Hassan, ameliambia gazeti hili kuwa, uchaguzi huo umepangwa kufanyika katika ukumbi wa EACROTANAL mjini Zanzibar.

Alisema uchaguzi huo utatanguliwa na kazi ya upitiaji fomu, upitishaji wa majina ya wagombea na usaili ambayo itafanyika Agosti 26 mwaka huu.

Alifahamisha kuwa, usaili wa wagombea utafanyika katika ukumbi wa Mafunzo, na kuongeza kuwa, wale watakaofaulu ndio watakaoingia katika kinyang’anyiro hicho kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Hadi sasa, alisema wagombea 17 wamejitokeza kuchukua fomu, sita kutoka Pemba na 11 kutoka Unguja, ambao wameomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Idadi ya wagombea hao bila ya kutaja majina, ni nafasi ya Rais (2), Makamo wa Rais Unguja (2) na Pemba wawili, Katibu (3), Katibu Msaidizi Pemba na Unguja wawili kila upande, Mshika Fedha wagombea wawili na wasaidizi wanne, ambapo wawili wametoka Unguja na wengine Pemba.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.