Habari za Punde

Mgombea wa CCM Jimbo la Bububu Hussein Makungu Bhaa Achukua Fomu Tume ya Uchanguzi Zanzibar.

MSIMAMIZI wa Uchaguzi mdogo Jimbo la Bububu , Ali Rashid Suluhu (kulia) akimkabidhi fomu Mgombea Uwakilishi katika Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Hussein Ibrahim Makungu (Bhaa) wakati mgombea huyo alipofika katika ofisi za tume ya Uchaguzi (ZEC) Wilaya ya Magharib zilizopo Maisara Mjini Unguja 



 Akitoka katik Ofisi za Tume baada ya kukabidhiwa Fomu ya Kugombea Jimbo la Bububu, baada ya kuwa wazi baada ya kufariki kwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Salimu Mtondoo. 
 Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Bububu kwa tiketi ya CCM Hussein Ibrahim Makungu, akiwapungia Wananchi mikono akiwa na Fomu yake ya Kugombea Uwakilishi Jimbo la Bububu baada ya kuchukua fomu hiyo Tume ya Uchanguzi Zanzibar, akipita katika mitaa ya Mjini wa Zenj akielekea Jimboni kutafuta wadhamini.
 Mgombea Uwakilishi kupitia Chama Cha Mapinduzi Hussein Ibrahim Makungu, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Bububu baada ya kuchukuwa Fomu ya kugombea Nafasi hiyi kwa Tiketi ya CCM, akiwa katika Ofisi ya Jimbo Bububu.  


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.