Habari za Punde

HISTORIA FUPI YA SHA HIGH SCHOOL

Wazo la kuanzishwa kwa Skuli hili lilibuniwa na Ndugu Ahmada na  kuliwasilisha kwa washirika  wake  ambao ni Kampuni ya SHA kirefu cha neno SHA ni :-  S – Saidi,   H – Hassan ,   A- Ahmada ambayo ni Kampuni iliyoanzishwa mwaka 1989,   baada kuridhiwa wazo hilo  liliwasilishwa Serikalini na bila ya khiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kujali uzalendo   ilitupa ardhi kwa moyo mkunjufu.

Mara baada ya kupata ardhi  hii Ujenzi ukaanza mara moja, katika harakati hizo Skuli imewekwa jiwe la msingi tarehe 9 -1 -2007 na aliekuwa Raisi wa Zanzibar  Mh, Amani A. Karume na ameifunguwa tarehe 18 -6-2010.          

Skuli ina usajili No. 318.  

Masomo yameanza rasmi tarehe 1 -02-2011.

Skuli imeanza na madaraza 9 kuanzia darasa la tano hadi la 14 (F.VI) chini ya Uongozi wa Nd. Zagu H. Zagu M/Mkuu wa kwanza.


Mwaka jana 2011 kwa mara ya kwanza wanafunzi wetu walifanya mtihani wa Taifa wa F.IV.

Ingawa ulikuwa ni mwaka  ambao watahiniwa wengi walifutiwa matokeo, lakini kwetu hakuwepo aliefutiwa. Matokeo yalikuwa kama yafuatayo:-

DIV - I hakuna,  DIV – II hakuna, DIV – III 3, DIV –IV -39, DIV - 0 6, jumla  W`ke 21 na W`ume  27 jumla 48  kwa watahiniwa wa  Skuli

( School candidates)  

Watahiniwa wa Private  candidates Matokeo yalikuwa kama  yafuatayo:-

DIV – I hakuna ,     DIV – II hakuna,    D – III  hakuna,   DIV - IV  80, DIV – 0  18.

Pia Skuli hii katika mwaka 2010 ilichukuwa wanafunzi wa darasa la F.V  idadi yao 6  wanawake 3 na wanaume 3  na kuendelea nao na masomo mpaka F.VI.

Mnamo mwezi wa Februari 2011 walifanya mtihani wa Taifa, waliofaulu wanafunzi  4 wakiume 3 na wakike 1, watatu kati yao wamepata sifa za kujiunga na Chuo mmoja,  wakiume  amepata cheti na wawili hawakufaulu  hii inadhihirisha wazi namna skuli  inavyojizatiti kuinua kiwango cha elimu  na kuimarisha elimu visiwani na Tanzania kwa jumla.

Hivi sasa Skuli ina wanafunzi 452 W`ke  202 na W`me 250, Walimu 24,  W`ke 8, na W`me 16, Kaimu  Mw/Mkuu ni Ndugu Moh`d A. Mussa. Wanafunzi wa F-IV ni 120 W`ke 54 na W`me 66, ambao wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa  mwezi wa Oktoba 2012.

MATARAJIO.

Matarajio yetu ni kama ifuatavyo:-

1.   Kurejesha usafiri wa wanafunzi  ambao ulisimama kutokana na tatizo la malipo suala ambalo tutalirekebisha baada ya kuonana na wazee.

2.   Kufanya mchujo wa wanafunzi wanaoingia kidato cha nne ili kuondoa wingi wa wanafunzi wa F.IV ambao hawana sifa.

3.   Kurejesha darasa la “A” Level kwa kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano (F.V) mwakani 2013.

4.   Kuandaa vijana wetu katika matumizi ya lugha zaidi ya mazungumzo kwa kuanzisha kituo cha mafunzo ya lugha mbali mbali zaidi ya kingereza. Katika kufundisha tutatumia CDS, DVD pia kutakuwa na  Discussion, debate n.k.

MWISHO

    Tunakuomba Mama yetu,  Mpenzi wetu, Dada yetu Mhe: Naibu Waziri  WEMA  BI ZAHRA ALI HAMAD  uwe mlezi wa Skuli hii.

3 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Salaam
    Naomba hizi takwimu ziwekwe sawa hapa. Habari inasema
    "Mwaka 2011 wanafunzi waliofanya mtihani wa F4 walikuwa 146.

    Matokeo yalikuwa kama yafuatayo:-

    DIV - I hakuna, DIV – II hakuna, DIV – III 3, DIV –IV -39, DIV - 0 6, jumla W`ke 21 na W`ume 27 jumla 48

    Sasa wanafunzi waliofanya mtihani ni 146 au 48?

    ReplyDelete
  3. Hii taarifa tulipewa na Uongozi wa Skuli hata hivyo baada ya kuipitia kwa kituo kweli inahitajia marekebisho. Hivyo tumeondoa kipengele ambacho kina mushkeli katika idadi ya wanafunzi.

    Ahsante mdau kwa kutanabahisha

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.