Jumla ya Washiriki 40 wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 ambao wapo Kambini Ikindoleo Lodge Hoteli ya kitalii, Kesho wataungana na wanavyuo mbalimbali Tanzania katika safari yao kwenda Bagamoyo kutangaza vivutio vya Utalii wa Ndani ya nchi, Safari hiyo ambayo inakwenda kwa jina la Tanzania Journalism Endorses Domestic Tour, Washiriki hao wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 ndio ambao watazindua Rasmi safari hizo ambazo zitaanzia Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na kisha kuwa wageni Rasmi katika Safari hiyo huko Bagamoyo.
Akizungumza na waandaaji wa Safari hiyo Rais wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Gideon Erasto Chipungahelo alisema fainali za Miss Utalii Tanzania kwa mwaka 2012/13 zitafanyika hivi karibuni. Pia amesema kwamba Miss Tourism Organisation wanatambua sana mchango wa wanafunzi wa vyuo mbalimbali Tanzania pamoja na waandishi wa Habari kwa hiyo imetoa sapoti kubwa kwa kuwaleta Warembo wote 40 kushiriki na wanafunzi hao katika Safari hiyo.
Katika safari hiyo ambapo wanafunzi wa vyuo vya DSJ,UDSM, TIA, IFM, TSJ, KIU, CBE, Open University Pamoja na vyuo vinginevyo watakuwepo.
Baadhi ya Maeneo watakayo tembelea kesho ni pamoja na Kaole Ruins, Mamba Ranch, Stone Town na Kanisani.

No comments:
Post a Comment