-
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza na wawakilishi wa makundi ya jamii ya watu wenye ulemavu ukiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. David Nyendo (kushoto) mara baada ya kufika katika makao makuu ya Tume leo (jumatano Feb. 13, 2013) kuwasilisha mapendekezo yao juu ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii ya watu wenye ulemavu. Wa pili kushoto ni Mjumbe wa Tume, Dkt. Salim Ahmed Salim
-
Mkalimani wa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu wa kusikia kutoka Umoja wa Miradi ya Viziwi Tanzania (UMVITA), Bi. Ruth Hope akisaidia uelewa wa lugha ya mawasiliano kwa watu wa jamii ya walemavu wa kusikia katika mkutano baina yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Walemavu hao waliunda kamati iliyokutana na Tume ili kuwasilisha mapendekezo yao juu ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii yao.
(PICHA
NA TUME YA KATIBA)
No comments:
Post a Comment