Kutoka kwa ‘Abdullah Ibn ‘Abbass,
Allah awawie radhi yeye na baba yake, amesema:-
" فرض رسول الله صلى الله
عليه وسلم زكاة الفطر طهرة للصائم من اللغو والرفث وطعمة
للمساكين من أداها قبل الصلاة فهي زكاة مقبولة ومن أداها بعد الصلاة فهي صدقة
من الصدقات
“Mtume Swalla Allahu ‘alayhi
wasallam amefaradhisha Zakaatul Fitr kwa wale waliofunga ili iwatoharishe
na yale mambo ya kipumbavu na maneno machafu (waliokuwa
wakifanya na kuongea wakati wa kufunga) na pia kwa wale maskini wapate
kulishwa. Yeyote mwenye kuitoa kabla ya sala basi hiyo ni
Zakaah iliokubalika , na mwenye kuitoa baada ya sala itahesabika
kama ni sadaqa miongoni mwa sadaqa”
Imepokewa na
Abu Daaud, Ibnu Majah na Ad daaru Qutniy
Imepokewa na Imaam Annawawiy
kwamba Wakii bin Al Jaraah amesema:
زَكَاةُ
الْفِطْرِ لِشَهْرِ رَمَضَانَ كَسَجْدَتِي السَّهْوِ لِلصَّلاةِ تَجْبُرُ
نُقْصَانَ الصَّوْمِ كَمَا يَجْبُرُ السُّجُودُ نُقْصَانَ الصَّلاةِ .،
Mfano wa Zakaatul Fitr kwa Ramadhaan ni sawa na mfano wa
Sijdatu Ssahw kwa Sala. Zakaatul fitr huikamilisha funga kama Sijdatus Sahw
inavyoikamilisha Sala kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.
No comments:
Post a Comment