Mheshimiwa Rashid Seif Suleiman akitoa hotuba yake
katika uzinduzi wa kituo cha umeme Cha Zoni ya Kaskazini.
Wasoma utenzi, Asha Haji kulia na Mwajuma wakighani
katika ufunguzi wa kituo cha umeme Zoni ya Kaskazini - Gamba
Mheshimiwa Rashid Seif
Suleiman akijiandaa kukata utepe na kufungua rasmi kituo cha utoaji huduma za
jamii cha zoni ya Kaskazini kilichopo Gamba, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Waziri wa Miundo Mbinu
na Mawasiliano, Mhe: Rashid Seif Suleiman akisalimiana na Meneja Mkuu wa
Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk alipowasili katika ufunguzi
wa kituo cha Zoni ya Kaskazini kilichopo Gamba, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Na ZECO
WANANCHI wamepewa elimu ya kununua taa (bulb) zenye kutumia
umeme mdogo (energy server) ili kupunguza matumizi makubwa ya umeme na
kupunguza gharama kubwa ambayo wananchi wanaitumia kwa kulipia umeme.
Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Rashid Seif Suleiman aliyasema hayo wakati
akifungua kituo cha umeme cha zoni ya Kaskazini kilichopo Gamba ikiwa ni
miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kuwa, ghara za umeme wakati mwengine
huongezeka zaidi kutokana na wananchi kutumia taa zenye kutumia umeme mkubwa
ambazo taa moja unaweza kutumia kwa taa nyingi zenye kutumia umeme mdogo
(energy server) inagawaje bei yake iko juu zaidi.
“Na sisi wananchi tuwapige chenga ZECO kwa kutumia
balbu zinanzotumia umeme mdogo, ingawaje bei yake ni ghali zaidi kuliko zile zinazotumia
umeme mkubwa lakini tuweke kidogo kidogo kwani balbu moja ya bei rahisi unaweza
kutumia balbu takriban saba (7) zinazotumia umeme mdogo hii itapunguza
gharama”. Alisema Mheshimiwa Waziri.
Aliwaeleza wananchi wa Mkoa wa Kaskazini kuweza
kikitumia kituo hicho kilichopo Gamba ili kukipa uhai kituo hicho na kusema ya
kuwa matumizi ya umeme ni nafuu sana kulikoni ya nishati nyengine.
Aidha, Mheshimiwa Waziri aliwataka wananchi kuweka
kumbu kumbu za risiti za malipo yao ili kuondoa migogoro kwa wananchi na
Shirika la umeme.
Kwa upande mwengine Mheshimiwa Rashid ametoa ahadi ya
kuishuhulikia bara bara ya njia hiyo kutoka Chaani Kikobweni hadi Gamba kipande
ambacho kinaonekana kimekuwa kibovu kwa kuwa na mashimo mengi.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na
Nishati, Mustafa Aboud Jumbe amesema kituo hicho kimerejeshwa kutoa huduma
baada ya kusita kutokana na kuwosogezea karibu wananchi wa Mkoa huo huduma za
umeme.
Nao wananchi wa Mkoa huo wamelipongeza Shirika la
Umeme kwa kufungua kituo hicho kwani kimeweza kuwapunguzia masafa ya kufuata
huduma mjini.
Kituo hiki kinatoa huduma za kiufundi za umeme, malipo
ya umeme kwa mita za kawaida na huduma za kuwasajili wateja wapya.
Shirika la Umeme (ZECO) katika kuadhimisha miaka hii
50 ya Mapinduzi ya Zanzibar limeweza kufungua miradi mitano (5) tokea shamra
shamra za maadhimisho ya miaka 50 zianze. Miradi iliyofunguliwa ni mitatu kwa
upande wa kisiwani Pemba na miwili kwa upande wa Zanzibar.
Miradi hiyo ni uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa
njia mpya ya umeme kisiwa cha Makoongwe, ufunguzi wa mradi wa umeme kijiji cha
Kichaka, ufunguzi wa ujenzi wa njia mpya ya umeme Ukunjwi ambayo yote hii ni kwaupande
wa Pemba na ufunguzi wa kituo cha utoaji huduma za kiufundi kwa jamii zoni ya
Kusini (Makunduchi) na zoni ya Kaskazini (Gamba).
No comments:
Post a Comment