Na Ally Ndota
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, leo
anatarajia kuanza ziara katika wilaya
zote 12 za mikoa sita ya kichama ya Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,
Dk. Shein, ataanza ziara hiyo kwa kutembelea
wilaya ya Mjini.
Lengo kuu la ziara hiyo, pamoja
na mambo mengine, ni kubadilishana
mawazo na uzoefu juu ya masuala ya kisiasa, ujenzi na uimarishaji wa chama
hicho na viongozi wa mashina wa wilaya
ya hiyo.
Atakamilisha ziara yake hiyo, mkoani
humo Novemba 19, ambapo atazuru wilaya
ya Amani na siku inayofuata, atatembelea wilaya ya Dimani, Mkoa wa Magharibi.
Atahitimisha ziara yake hiyo
Disemba 4, mwaka huu, ambapo atabadilishana mawazo kuhusu uimarishaji wa chama
na mabalozi wa wilaya ya Mkoani, mkoa wa
kusini, Pemba.
Katika ziara hiyo, atafuatana
na viongozi mbali mbali wa chama hicho, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-
Zanzibar, Vuai Ali Vuai pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya
NEC Zanzibar.
No comments:
Post a Comment