Habari za Punde

Timu ya Mwembeladu yachanja mbuga Nane bora ligi daraja la Pili




Timu ya Daraja la pili ya Mwembeladu mjini Unguja inaendelea vizuri katika mashindano ya nane bora kutafuta timu mbili zitakazopanda daraja baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo.

Mechi ya kwanza waliwafunga Majirani wao Timu ya Kundemba 2-0  na jana usiku waliweza kuwafunga timu ya Vikokotoni  3-0.

Hongera Kocha Masoud Chile  kwa ushindi wapili mfululizo katika  nanebora ligi daraja la pili Zanzibar ambapo timu ilionesha kandanda safi la kutoka kitabuni lililofundishwa na Kocha Chile.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.