Bendera ya Palestine itapepea nje ya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, hii inafuatia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio ambalo linatoa fursa kwa nchi ambazo si mwanachama kamili wa Umoja huo kupeperusha bendera yake Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Ubao wa Matangazo ndani ya Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ukionyesha matokeo ya kura katika tukio la kihistoria kufanyika ambapo Baraza hilo limepitisha azimio linalotoa fursa kwa Palestina kupeperusha bendera yake. Nchi wanachama walipiga makofi kushangilia kupitishwa kwa azimio hilo, ambalo Israel imesema Palestina inatafuta umaarufu kwa njia za mkato badala ya kurejea kwenye meza ya mazugumzo.
Na Mwandishi Maalum New York
Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, jana Alhamis, limepitisha Azimio
ambalo kwa mara ya kwanza tangu
kuanzishwa kwa Umoja huo, litaruhusu nchi ambazo siyo mwanachama
kamili kupeperusha bendera yake
katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Kupitishwa kwa azimio hilo
ambalo limepigiwa kura za ndiyo 119 za hapana nane
na zisizofungamana na upande wowote 45 kunaipa fursa Palestina kupeperusha bendera yake nje ya Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa.
Mara baada ya matokeo ya kura kutangazwa rasmi, Wajumbe wa
Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa walipiga makofi kama ishara ya kufurahia kupitishwa kura nyingi
azimio hilo.
Palestina kama ilivyo kwa Vatican inahadhi ya Nchi
Mwangalizi isiyo Mwanachama wa Umoja wa Mataifa (Non -Member Observer States)
Kwa mujibu wa Azimio hilo nambaA/69/L.87 linaloelezwa kuwa
ni la kihistoria, linamtaka Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha kwamba Bendera ya Palestina inapeperushwa ndani ya siku 20 ( septemba 30)wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu
la 70 la Umoja wa Mataifa.
Akiwasilisha azimio hilo mbele
ya wajumbe, Mwakilishi wa Kudumu wa Iraq na ambaye ni mwenyekiti wa kundi la nchi
za kiarabu alisema kupeperushwa kwa
bendera ya Palestina ni kielelezo cha utekelezaji wa matakwa yaliyomo ndani
ya Katiba ya Umoja wa Mataifa ya kwamba,
nchi zote na watu wake wako sawa na wana haki
sawa.
Hata hiyo si mataifa yote
yaliyoridhika ya uamuzi huo, kwa kile ambacho wengine wameeleza kuwa ni
ukiukwaji wa kanuni za Umoja wa Mataifa
ambazo zinaeleza wazi wazi kwamba bendera zinazopashwa kupeperushwa katika Umoja wa Mataifa ni zile tu za nchi ambazo ni wanachama kamili.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kudumu wa Israel katika Umoja
wa Mataifa, yeye alisema kwamba kupeperushwa kwa bendera ya Paletina katika Umoja wa Mataifa, hakubadilishi hali halisi
na mazingira ya sintofahamu yanayoendelea kati yake na Palestina.
Akizungumza kwa hisia kali
huku akizilaumu nchi ambazo zimeunga mkono azimio hilo, Mwakilishi huyo
wa Israel, ameeleza kwamba Palestina inatakiwa kufanya maamuzi magumu yakiwamo
ya kurejea katika meza ya mazungumo
badala ya kutafuta njia za mkato
zikiwamo hizo za kupeperusha
bendera katika Umoja wa Mataifa.
Akasema yeye kama mwakilishi wa Israel picha ambayo
anaamini ndiyo inayostahili kuwa maarufu ni ile ya viongozi wa Israel na
Palestine watakapokuwa kwa pamoja wanapandisha bendera ya matumaini inayoonesha mataifa hayo mawili yakiishi kwa pamoja kwa Amani na usalama.
Hoja ya kutaka Israel na Palestina kurejea kwenye
mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu baina ya pande hizo mbili imeungwa mkono na wazungumzaji wengi wakiwamo
wale waliopiga waliopiga kura ya hapana
kama vile Marekani .
Kwa upande wa wale waliounga mkono azimio hilo,
walieleza kwamba nchi inapo peperusha bendera yake hata ni kielelezo cha ufahari, utambulisho na
uwepo wake na kwa sababu hiyo Palestine ilikuwa na kila sababu ya kupeperusha bendera yake ambayo kwayo
haibadilishi hadhi yake ya kuwa nchi mwangalizi, lakini ikiandika historia
nyingine.
Mwakilishi wa Palestina akiwa
na furaha tele amezishukuru nchi zote
ambazo zimeunga mkono azimio hilo.
Pamoja na kupitishwa kwa Azimio hilo linalotoa fursa
kwa nchi ambazo si wanachama kamili kupeperusha bendera,
Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa pia walipitisha kwa kupiga kura
azimio linalotaka kuangaliwa kwa misingi ya utaratibu wa marekebisho ya ulipaji wa madeni kwa nchi zinazodaiwa.
Azimio hilo namba A/69/L.84 lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Kundi la Nchi 77 na China (
G77&China) lilipita kuwa kura 136 za ndiyo, sita za hapa na 41 zisizofungamana na upande wowote
No comments:
Post a Comment