MKUTUBI wa Maktaba Kuu ya Pemba Azida Salim Juma,
akiwawagawia wanafunzi 60 wa skuli ya kojani msingi Vitabu, katika mikakati ya
kuwahamasisha wanafunzi kupenda kusoma vitabu, wakati wa utekelezaji wa mradi
wa SIDA.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Kojani wakisoma vitabu
baada ya kupatiwa na wafanyakazi wa Makatba kuu ya Pemba, katika utekelezaji wa
mradi wa kuhamasisha wanafunzi maskulini Pemba kusoma unaofadhiliwa na SIDA.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WANAFUNZI wa skuli ya kojani Msingi wakionesha
vitabu vyao walivyopatiwa na wakutubi wa maktaba kuu ya Pemba, kupitia mradi wa
SIDA, ambao unahamasisha wanafunzi kupenda kusoma vitabu.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MMOJA wa Wanafunzi wa skuli ya msingi Kojani akisoma
kitabu cha hadithi, alichopatiwa na wakutubi wa maktaba kuu ya Pemba, katika
utekelezaji wa mradi wa SIDA wenye lengo la kuhamasisha wanafunzi kupenda
kusoma vitabu.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
WANAFUNZI wa skuli ya Kojani msingi wakichora picha
mbali mbali katika utekelezaji wa mradi wa SIDA, wenye lengo la kuhamasisha
wanafunzi wa skuli za msingi kupenda kusoma vitabu.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
he! watoto wa skuli wapo kwenye mjamvi kama chuoni, dah masikini Zanzibar
ReplyDelete