Habari za Punde

Mafunzo ya haki za binadamu kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi yafanyika kisiwani Pemba

 AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed akielezea jinsi kituo hicho kinavyotoa huduma za kisheria, wakati wa mafunzo ya haki za binadamu yaliofanyika kituoni hapo mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WASHIRIKI wa mafunzo wa haki za binadamu ambao ni watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Pemba, wakisikiliza utoaji wa mada kwenye mafunzo hayo yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika mjini Chake chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MRATIBU wa Tume ya ukimwi Pemba ZAC Nassor Ali Abdalla akifungua mafunzo ya siku mbili ya haki za binadamu kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ZAPHA+ kulia ni Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLASC na kushoto ni mfanyakazi wa kituo hicho Asya Awadhi Ahmed, (Picha na haji Nassor, Pemba).
 AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Khalfan Amour Mohamed, akiwasilisha mada ya haki za binadamu kwenye mafunzo yaliowashirikisha watu wanaoishi na VVU Pemba, mafunzo yaliofanyika mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MWANACHAMA  wa Jumuia ya watu wanaoishi na VVU Pemba Fatma Said Rashid akiuliza suali kwenye mafunzo ya haki za binadamu yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar tawi la Pemba na kufanyika afisini kwao mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassot, Pemba).
MSHIRIKI wa mafunzo ya haki za binadamu Sabri Issa, akiuliza suali kwenye mafunzo hayo yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba na kufanyika afisini kwao mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassot, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.