Habari za Punde

Mhe Mohammed Raza Akabidhi Misaada kwa Waathirika wa Maafa ya Mvua Zanzibar na Kambi ya Kipindupindu.

Mhe Mohammed Raza akikabidhi Msada wa Vyakula kwa Mkuu wa Kambi ya Wananchi Waliopata Maafa ya Mvua Bi Rahma Kassim Ali, makabidhiano hayo yamefanyika katika kambi hiyo iliokuweko Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja. 

 Mfanyabiashara na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar Mhe Mohammed Raza akizungumza na waandishi wa habari kutokana na msaada aliokabidhi kwa wananchi wanaoishi katika kambi hiyo amekabidhi Mchele, Sukari, Chupa za Chai, Maji na bidhaa nyengine.
Mkuu wa Kambi ya Wananchi walioathirika na Mvua za Masika katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja Bi Rahma Kassim Ali, akitowa shukrani kwa Mfanyabiashara na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar kwa msaada wake kwa Wananchi wanaokaa katika kambi hiyo kutokana na Nyumba zao kuingia maji na kukosa pahali pa kukaa. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.