Habari za Punde

Balozi Seif awafariji wahanga wa kisiasa kisiwani Pemba

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Ndugu Said Khamis Mohammed wa Kijiji cha Shengejuu aliyehujumiwa Nyumba na mali zake zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 5,610,000/- kwa sababu za itikadi za Kisiasa.
  Nyumba ya Ndugu Said iliyopo katika Kijiji cha Shengejuu inayoonekana kuharibiwa vibaya pamoja na kun’golewa
madirisha  yake yote hujuma iliyofanywa kwa sababu za itikadi za kisiasa.
 Mkuu wa Wilaya ya Wete Nd. Rashid Hadid wa pili kutoka kulia akimpatia maelezo Balozi Seif kuhusu hujuma alizofanyiwa mwananchi Said Khamis na hatua za awali zilizochukuliwa na Ofisi ya Wilaya katika kukabiliana na vitendo vya hujuma.
  Balozi Seif akimfariji Mfanyakazi wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga chapa Mkuu wa Serikali Kisiwani Pemba NduguKai Shaame Kai Nyumbani kwake Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kushambuliwa kwa virungu na mikwaju na watu alipofika bandarini Kiuyu Micheweni kupata huduma za samaki.
 Balozi Seif akimpa pole Bibi Raya Yussuf Hamadi Mzazi wake Ndugu Said Khamis wa Kijiji cha Shengejuu aliyepigwa jiwe zito kifuani kwa sababu za Kisiasa na kusababishia maumivu makali yaliyopelekea kulazwa Hospitali ya Wete kupatiwa matibabu.

Sheha wa Shehia ya Maziwang’ombe Bibi Asha Yussuf Hamadi akifarijiwa na kupewa pole na Makamu wa ili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kuvamiwa usiku wa manane kwa lengo la kuhujumiwa.
 Nyumba ya Sheha wa Shehia ya Maziwang’ombe Bibi Asha Yussuf iliyobomolewa sehemu ya nyuma na kikundi cha watu  kwa sababu za kisiasa na kumsababishia hasara kubwaNo comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.