Habari za Punde

Dk Shen afanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:

1.                 UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 61(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:
i.                    Mkuu wa Mkoa wa Mjini na Magharibi – Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud

ii.                  Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja – Mheshimiwa Vuai Mwinyi Mohamed

Aidha Wakuu wa Mikoa ambao Mikoa yao haikutajwa katika taarifa hii  wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 23 Mei 2016.

2.                 UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 61(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:
  i.  Mkuu wa Wilaya ya Mjini – Mheshimiwa Marina Joel Thomas.


 ii.   Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” – Mheshimiwa Silima Haji Haji

 iii.    Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A”– Mheshimiwa Hassan Ali Kombo
  iv.  Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” – Mheshimiwa Issa Juma Ali

  v.  Mkuu wa Wilaya ya Kati  – Mheshimiwa Mashavu Sukwa Said

  vi. Mkuu wa Wilaya ya Kusini – Mheshimiwa Idrissa Kitwana Mustafa
  vii. Mkuu wa Wilaya ya Chakechake – Mheshimiwa Salama Mbarouk Khatib

Aidha Wakuu wa Wilaya ambao Wilaya zao hazikutajwa katika taarifa hii  wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 23 Mei 2016.

Viongozi wote waliotajwa wanatakiwa waripoti Ikulu, Mjini – Unguja, siku ya Jumanne tarehe 24 Mei 2016 saa 8 za mchana tayari kwa kuapishwa.


(DKT. ABDULHAMID Y. MZEE)
KATIBU  WA BARAZA LA MAPINDUZI
NA KATIBU MKUU KIONGOZI,
ZANZIBAR.

23 MEI, 2016


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.