Habari za Punde

Kijana afariki kutokana na kipigo kutoka kwa watu wasiojulikana

Na Salmin Juma, Pemba

Kijana mmoja amekutwa akiwa amesha fariki huko ndugu kitu wilaya ya chake chake Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa watu wasio julikana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba  Shekhan Mohd Shekhan amesema kuwa marehemu Ibrahim Hija Kipenda (28) mkaazi wa msingini chake chake  wamemkuta akiwa tayari amesha fariki kutokana na kipigo hicho alichokipata kwa watu hao.

Amefahamisha kuwa katika uchunguzi wa awali wamebaini kuwa kijana huyo imeonyesha alishambuliwa sana na kupelekea kupata  namejeraha makubwa katika mwili wake.

Ameeleza kuwa marehu huyo alibainika kukutwa na  nazi kwenye polo pamoja na matunda mengine anayodaiwa kuwa aliyaiba kwenyeshamba la mtu ambae hakujulikana.

 Kwaupande wake Daktari dhamana wa Hospitali ya Chake chake Habibu Khamis amekiri kupokelewa mwili wa  merehem huyo na uchunguzi umebainisha chanzo cha cha kifo chake nikutokana na  majeraha makali aliyoyapata  ikiwa nipamoja na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kinachozaniwa kuwa ni kisu.

Nae mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mh. Salama Mbarouk Khatib amesema kuwa walipata taarifa ya kuonekana kwa marehemu huyo wakati wakiwa katika maandalizi ya ziara rasmi ya Rais wa Zanzibar hapa Kisiwani Pemba.

Amefahamisha kuwa kwakushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama vya Mkoa wa Kusini Pemba waliweza kufika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka hospitali ya Wilaya ya Chake Chake kwa uchunguzi baadae mwili huwo kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa mazishi.

Aidha ameitaka jamii kuto jichukulia sheria mikononi mwao nabadala yake wafuate sheria ili kuweza kuwafikisha katika vyombo vya maamuzi wale wote wanaogundulika kutenda makosa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.