Habari za Punde

Kamati ya Maendeleo Wanawake Habari na Utalii Yaendelea na Ziara Yake Kisiwani Pemba Yatembelea Kituo cha ZBC TV Pemba.,

Wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya baraza la wawakilishi, wakiangalia mitambo ya Kisasa ya ZBC TV huko mkoroshoni, wakati wa ziara yao ya kutembelea taasisi mbali mbali za zilizomo chini ya Wizara ya Habari
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC TV ) Kituo cha Pemba, wakiwa katika harakati za kutayarisha habari za Pemba, kwa lengo la kuzituma ZBC TV Unguja.
Moja ya Studio za kurushia matangazo ya kisasa ya ZBC TV kituo cha Pemba, baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa na kukwa vifaa vya kisasa katika kituo hicho
Waziri wa Habari Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe.Rashid Ali Juma akiwakaguza maeneo ya kituo cha TV Pemba, wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati wa ziara ya wajumbe hao Pemba
Mratibu wa ZBC TV Pemba, Khamis Ali akisoma taarifa ya kituo cha TV kwa wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii, wakati walipotembela kituo hicho ZBC TV Mkoroshoni Chake Chake Pemba
MWENYEKITI wa kamati ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ali Suleiman Shihata akiangalia ramani ya ujenzi wa jingo la ZBC TV, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wake Salha Mohammed Mwinjuma na Kulia ni Naibu waziri wa Habari Zanzibar Chumu Kombo Khamis.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.