Habari za Punde

Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Azungumzia Mafanikio ya Benki Kwa Muhula wa Tatu wa Mwaka 2017.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd PBZ Juma Ameir Hafidh akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar mafanikio yaliopatikana kwa PBZ Kwa Muhula wa tatu kwa mwaka 2017, mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya PBZ mpirani Zanzibar.  
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidhi akisoma Taarifa ya Mafanikio ya Benki kwa muhula wa Tatu wa mwaka 2017, na kutoa m,aelezo faida iliopatikana kupitia huduma za kibenki kwa Wananchi wanaopata huduma hizo kupitia PBZ kwa Zanzibar na Tanzania Bara na kusisitiza zaidi ya Wafanyakazi wa SMZ na SMT wamechukua mikopo kupitia PBZ, mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya PBZ katika jengo la Shirika la Bima Mpirani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji Juma Ameir Hafidh akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari alipokuwa akitowa Taarifa ya mafanikio ya PBZ katika ukumbi wa Makao Makuu ya PBZ yalioko jengo la Shirika la Bima Mpirani Zanzibar. 
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidh akitowa taarifa kwa waandishi wa habari Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.