Habari za Punde

Balozi Seif atembelea taasisi zilizohamishiwa Ofisi yake

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiitembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Idara ya Mazingira zilizopo Maruhubi ambazo kwa sasa zipo chini ya Ofisi yake.
Kushoto ya Balozi Seif  Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Bibi Farhati Haji Mabarouk na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Nd. Haji Mjaja Haji.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Nd. Haji Mjaja Haij akito ufafanuzi wa majukumu ya Taasisi yake mbele ya Balozi Seif aliyefanya ziara katika Taasisi hiyo
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Bibi Farhati Haji Mabrouk akifahamisha jambo mbele ya Balozi Seif hapo kwenye Ofisi yao Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Balozi Seif  Kutoka Kushoto akiendelea na ziara yake katika Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa kwenye Kituo cha Operesheni na Mawasiliano kiliopo Maruhubi kujionea uendaji wa Taasisi hiyo muhimu kwa Taifa.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar aliyesimama Nd. Makame Khatib Makame akifafanua masuala mbali mbali mbele ya Balozi Seif aliyefika kuikagua Taasisi hiyo.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema suala la Tabia Nchi linaendelea kukumbwa na utata kutokana na baadhi ya Wanaadamu kudharau utunzaji wa mazingira kunakopelekea kuzuka kwa migogoro isiyokwisha Duniani.
Alisema yapo Mataifa mengi Duniani hasa yale machanga yanayoendelea yaliyoathirika na Tabia Nchi licha ya Mwenyezi  Muungu kuiumba Dunia yenye neema na kuwaumba Wanaadamu wazuri lakini baadhi yao wamekuwa asi katika kuchafua mazingira.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira na wale wa Idara ya Mazingira  baada ya kutembelea Taasisi hizo hapo Maruhubi ambazo kwa sasa zimehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Alisema mienendo ya Miongo ya hali ya Hewa hivi sasa imepanguka sambamba na mipangilio ya Kilimo iliyobadilika kufuatia Wanaadamu kukosa huruma katika matumizi ya mali zisizorejesheka na hatimae uchafuzi wa mazingira umeongezeka kwa asilimia kubwa .
Balozi Seif alifahamisha kwamba zipo Nchi zinazoendelea na Maisha ya kawaida kwa kupata baraka ya mvua kutokana na kuheshimu mazingira yao hasa utunzaji wa Miti akilitolea mfano Taifa ya Jamuhuri ya Cuba.
Aliwakumbusha Watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira pamoja na Idara ya Mazingira kuendelea kutekeleza wajibu wao wa kusimamia utunzaji wa Mazingira ili Jamii iweze kustawika vyema.
Balozi Seif alisisitiza pia umuhimu wa kusimamia Sheria ya kupiga vita marufuku ya uingizaji wa Mifuko ya Plastiki Visiwani Zanzibar kwa lengo la kuepuka athari kubwa ya Kimazingira.
Akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar baada ya kutembelea Kituo cha Operesheni na Mawasiliano cha Maafa kiliopo Maruhubi Balozi Seif alisema Taasisi hiyo inasimamia jukumu lisiloonekana jambo ambalo watendaji wake wanapaswa kuwa tayari wakati na saa ye yote pale inapotokezea janga la ghafla.
A lisema Jamii ni vyema ikajenga Utamaduni wa kuwa na Imani kwa Watendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa  wakati wanapokumbwa na Maafa katika maeneo yao wanayoishi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Viongozi na Watendaji wa Taasisi hiyo kwa kazi nzuriwanazozifanya ambazo zimeleta faraja kwa Serikali Kuu.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelazimika kuimarisha zaidi Kitengo cha kukabiliana na Maafa baada ya kupata funzo kubwa lililotokana na maafa ya ajali mbili za Meli ile ya Spice Islan na M.V  Skajit miaka michache iliyopita na kuleta simanzi kubwa miongoni mwa Jamii na Taifa kwa ujumla.
Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar Nd. Haji Mjaja Haji alisema Taasisi hiyo hupokea Ripoti za Tathmini mbali mbali zipatazo 50 kwa Mwaka ainazohusiana na shughuli za Kimazingira.
Nd. Mjaja alisema Ripoti hizo pia zimefuatiliwa na zile zinazohusiana na masuala ya Mafuta na Gesi Asilia ambazo Taifa linalazimika kuwa makini katika kujiepusha mapema na athari kabla ya kusubiri matokeo mabaya hapo baadae.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukambiliana na Maafa Zanzibar  Nd. Makame Khatib Makame alisema Sekriterieti ya Kukabiliana na Maafa imekuwa ikifanya ukaguzi na Mipango ya Kukabiliana na Maafa ili kuepuka athari mapema.
Nd. Makame alisema vipo vyombo kadhaa vya Usafiri wa Baharini vilivyofanyiwa ukaguzi huo vikiwemo vituo vya Mafuta na kuridhika na Mazingira yaliyomo kwenye vyombo hivyo.
Alisema Ukaguzi huo umeenda sambamba na Daftari Maalum lililowekwa kuratibu Watu wanaokabiliwa na Maafa Kila Mwaka  ambapo Takwimu zinaonyesha uwepo wa Watu 51 waliofikia kigezo cha kuingia katika Daftari hilo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Taasisi hizo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdulla Hassan  Mitawi alisema Wizara hiyo imeziona changamoto zinazozikabili Taasisi hizo mbili na itafanya jitihada katika kuzitafutia ufumbuzi wakudumu.
Nd. Abdulla alisema Taasisi zinayosimamia Masuala ya Kimazingira zinastahiki kupewa kipaumbele kutokana na changamoto kubwa inayowakabili ya ufinyu wa Ofisi kwa Watendaji wao huku ikieleweka kubeba jukumu zito la Taifa la usimamizi wa Mazingira.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.