Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia
akisalimiana na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas
Domingo alipofika kwenye Makaazi yake Jijini Dar es salaam kumpongeza kwa Cuba
kumaliza Uchaguzi wa Rais salama.
Balozi Seif akitia saini Kitabu cha Wageni
mara baada ya kukaribishwa kwenye Ubalozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania
Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziabr Balozi
Seif Kulia na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Prifesa
Lucas Domingo Kushoto wakibadilishana mawazo kwenye Makaazi ya
Balozi wa Cuba Mjini Dar es salaam.
Balozi Seif na Profesa Lucan akiangalia baadhi
ya Picha na matukio mbali mbali yaliyojiri kwenye Maktaba ya Ubalozi wa
Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama
Asha Suleiman Iddi Kulia na Mke wa Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Mama Melyin
Suazez Alvarez Kati kati Wakimfanyia mzaha Mtoto wa Mke wa Balozi
Huyo aitwae Evelyn Hernandes Suarez.
Balozi Seif akiagana na Mke wa Balozi wa
Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Mama Melyin Suarez Alvarez.Kati kati yao ni Balozi Lucas Domingo
Hernandes na Mtoto wake Evelyn Hernandes Suarez.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi ameipongeza Jamuhuri ya Cuba kwa kumaliza Uchaguzi wa Bunge salama wa
kuwachagua Wajumbe wa Baraza Kuu la Nguvu ya Umma lenye Mamlaka ya kumchagua
Rais wa Baraza la Taifa la Nchi hiyo.
Alisema uchaguzi huo uliofanyika Mnamo Tarehe
11 Machi, 2018, ambapo Wajumbe wa Baraza la Taifa la Cuba
walimchaguwa Bwana Miguel Diaz –Canel kuwa Rais wa Nchi hiyo aliyekuwa msaidizi
wa Kiongozi wa Taifa hilo Bwana Raul Castro ulikuwa na amani na kushuhudiwa na
Jumuiya za Kimataifa.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa pongezi hizo
wakati akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas
Domingo Hernandes kwenye Makazi yake Jijini Dar es salaam.
Alisema kufuatia kumalizika kwa
uchaguzi huo Tanzania na Cuba zitaendelea kupata wasaa zaidi wa
kushirikiana katika masuala na sekta zilizoanzishwa ambazo ana matumaini ya
kuendelezwa chini ya Rais huyo Mpya wa Cuba Bwana Maguel Diaz – Canel mwenye
fikra za watangulizi wake waliolenga kuona ustawi wa Bara la Afrika unaimarika
na kukua siku hadi siku.
Akitoa shukrani zake Balozi wa Jamuhuri ya
Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernandes alimuhakikishia Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Cuba itaendelea kuiunga Mkono Tanzania hasa
katika masuala ya Elimu na Afya.
Profesa Lucas alisema miradi ya pamoja
iliyoanzishwa akiutolea mfano ule wa Afya umeanza kutoa sura ya matumaini
kufutia baadhi ya Madaktari Wazalendo wa Zanzibar kuendelea na mafunzo yao ya
Juu ya Udaktari Nchini Cuba baada ya kumaliza masomo yao Zanzibar chini ya
usimamizi wa Wataalamu na Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Matantas cha Nchini humo.
Kiongozi huyo Mpya wa Taifa la Cuba akiwa wa
Tatu tokea Taifa hilo kupata Uhuru wake alishika wadhifa huo kwa
kupata Asilimia 85.65% baada ya kushinda Viti Mia Sita na Tano.
Bwana Miguel Diaz – Canel wa Chama cha
Kikoministi anayeshika nafasi hiyo ya Urais katika kipindi cha Miaka Mitano akiendelea
hadi Mwaka 2023 amepungukiwa na Viti 7 ikilinganishwa na Uchaguzi uliopita wa
Mwaka 2013 ambapo mshindi aliibuka na Viti 612.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa salamu za pole kwa Rais wa Cuba Bwama Miguel
Diaz – Canel kupitia Balozi wa Nchi Hiyo Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo
kufuatia ajali ya Ndege ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Cuba { Cubana
Airlines }.
Ajali hiyo iliyotokea katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Havana wa Jose Marti ilisababisha idadi ya Vifo vya Abiria Mia
111 hadi kufikia mapema wiki hii ambao walikuwemo kwenye Ndege hiyo.
Balozi Seif kupitia Balozi huyo wa Cuba Nchini
Tanzania aliwataka Wananchi wa Cuba pamoja na wale wenye jamaa na ndugu zao
waliokumbwa na Umauti huo kuwa na moyo wa Subira katika kipindi hichi kizito
cha Msiba.
Alisema Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa
Ujumla wanaungana na Serikali ya Cuba pamoja na Wananchi wake katika msiba huo
uliojumuisha pia Vijana ambao ndio nguvu kazi iliyokuwa ikitegemewa na Taifa
hilo.
Ndege hiyo ya Abiria ilipata ajali mara baada
ya kuruka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jose
Marti katika Mji Mkuu wa Havana ikielekea Mji wa Holguin
ulioko Mashariki mwa Nchi hiyo.
Kwa mujibu wa takwimu za Vyombo vya Habari
hiyo ni ajali ya Tatu kubwa za Ndege Nchini Cuba tokea mnamo Mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment