Habari za Punde

PBZ Yakabidhi Msaada wa Vyakula Vituo Vya Watoto na Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar Kwa Ajili ya Futari.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Bi. Khadija Shamte Mzee akimkabidhi msaada wa Vyakula Mtoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibat Mtoto Abdulrahaman Abdallah kwa ajiliya matumizi yao ya futari akipokea baadhi ya vyakula hivyo.PBZ imekabidhi Sukari, Mchele, Unga wa Ngano na Mafuta ya kula, kwa ajili ya Futari.PBZ hutowa misaada kwa Jamii Zanzibar.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Bi. Khadija Shamta Mzee akiwa katika picha ya pamoja na Walezi na Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar baada ya hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo uliotolewa na PBZ.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Bi. Khadija Shamte Mzee akiwa na Maafisa wa PBZ na Walezi na Watoto wa nyumba hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla hiyo iliofanyika katika makaazi yao mazizini Zanzibar. 
Afisa Ustawi wa Jamii Katika Makaazi ya Watoto wa Nyumba ya Watoto ya Serikali Mazizini Zanzibar Ndg.Juma Makame Kombe akitowa neno la shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa Msaada wao huo na kuzitaka taasisi nyengine kuchukua fursa kutoa misaada kwa Watoto Yatima Zanzibar.Afisa Muandamizi wa Masoko wa PBZ Ndg. Anasi Rashid Ramadhani akipokea mkono wa shukrani kutoka kwa mmoja wa Watoto wanaoishi katika Nyumba ya Watoto Yatima Fuoni Markasi Fuoni Zanzibar.
Afisa Muandamizi wa Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited (PBZ) Ndg. Anasi Rashid Ramadhani akiwa katika picha ya pamoja na Mlezi na Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Markas Fuoni Ijitimai, baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya futari katika mwezi huo wa Ramadhani.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.