Habari za Punde

Rais wa ZFA ajiuzulu rasmi

                         Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina katikati
Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) Ravia Idarous Faina ameandika barua rasmi ya kujiuzulu nafasi yake na sasa wataungana na Makamo wa Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali na Mkurugenzi wa ufundi Abdulghan Msoma ambao walitangaza kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Mei, 2018.
 Katibu mkuu wa ZFA Mohammed Ali Hilali (Tedy) amethibitisha kupokea barua hiyo ya Ravia.
 “Ni kweli ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake, barua ameileta leo Jumatano saa 9 za mchana”. Alisema Tedy. Ravia alipokea kijiti hicho cha Urais kutoka kwa Amani Ibrahim Makungu mwaka 2013.
Yote hayo inawezekana ikawa sababu kufuatia Zanzibar kupitia timu yake ya Vijana ya Karume Boys kuondolewa katika Mashindano ya Cecafa ya Vijana yaliyofanyika hivi karibuni nchini Burundi ambapo Karume Boys licha ya kuondoshwa katika Mashindano pia walipigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo walikwenda kinyume na kanuni ya Mashindano.
 Kutokana na makosa hayo Karume boys imepewa adhabu tatu ikiwemo kuondolewa mashindanoni, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa kulipwa na Chama cha Soka la Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia gharama za tiketi, malazi na chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa Burundi huku adhabu ya tatu ikiwa kufungiwa kutoshiriki mashindano yanayoendeshwa na CECAFA hadi hapo watakapolipa faini hiyo ambayo inatakiwa kurudishwa FIFA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.