Habari za Punde

Taasisi ya IESC yatoa mafunzo ya mpira wa Kikapu Basket Ball kwa Walimu wa skuli na Makocha

 MKUFUNZI wa masuala ya Michezo kutoka IESC (International Education & Sport Consultant) akizungumza na Walimu wa mchezo wa Baskeli ball Maskulini na makocha wa mchezo huo, katika ukumbi wa Magofu juu ya sheria za mchezo huo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUFUNZI wa masuala ya Michezo kutoka IESC (International Education & Sport Consultant) akifundisha moja ya vitu vinavyohitajika wakati mchezaji anapotaka kufunga bao, wakati alipokuwa akitoa mafunzo ya siku mbili kwa Walimu na Makocha katika ukumbi wa Magofu juu ya sheria za mchezo huo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) 


NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

Tasisi ya IESC (International Education & Sport Consultant), imesema lengo la kuwepo Zanzibar ni kusaidia kufundisha walimu wa Zanzibar, ili kuweza kufanya vizuri katika masuala la Michezo.

Mkufunzi wa Masuala ya michezo kutoka Taasisi hiyo, Greg Sizemore, alisema wameamua kufundisha masuala ya michezo kwa walimu wa skuli za Serikali na Makocha wa Timu za Basket Ball, ili kuweza kuibua vipaji vya wachezaji wa mchezo huo kupitia maskulini.

Kauli hiyo aliitoa huko katika ukumbi wa Magofu Chake Chake Pemba, wakati alipokuwa akizungumza na walimu na makocha wa mchezo wa Basket Ball wa Wilaya hiyo, katika mafunzo ya siku mbili juu ya sheria za basket boll.

Alisema walimu hao licha ya siku kuwa mbili, lakini kama watachofundishwa watakifikisha maskulini na kwenye timu zao, basi mafanikio makubwa yatapatikana kupitia mchezo huo wa basket Ball.

“Kila mwaka tunafanya mafunzo kwa walimu wa michezo, kwa mwaka huu tumeamua kuwafundisha juu ya Basket Ball, ili vipaji vilivyoko Pemba viweze kuibuliwa na kuwaonyesha viwango vyao”alisema.

Kaimu Naibu Katibu Mkuu Baza Pemba, Stara Khamis alisema lengo la Baza ni kuhamasisha vijana kuupenda mchezo huo wa Basket Boll, ili Chake Chake kuwa wilaya ya Mfano na tishio katika kisiwa cha Pemba na Zanzibar kwa ujumla juu ya mchezo huo.

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi ambazo zinawakumba Vijana, lakini Serikali ya Mpainduzi ya Zanzibar imewapa kipaombele vijana, ili kufikia mbali zaidi kwa lengo la kukuza vipaji vya mbali mbali na kuviendeleza Tanznaia.

Alisema matarajio yao ni kuona Chake Chake inaibuka na ushindi katika mashindano mbali mbali, makubwa ikiwemo mchezo wa basket boll inafanya vizuri.

Mkurugenzi mkuu wa IESC Zanzibar Brizn Shonkwiler, alisema michezo ni muhimu sana kwa vijana kwani inafundisha Tabia njema, nidhamu, heshima na kufahamu kushindwa na kushinda.

Alisema wameamua kusaidia mchezo wa basket boll Unguja na Pemba, kwani vijana ndio nguvu kazi za taifa na vijana wa leo ndio vijana wa kesho.

Katibu wa timu ya Basket Boll ya Stone Town Hamad Heri, alisema mafunzo hayo kwa walimu na makocha wa Chake Chake, yataweza kuendelea kuibua vipaji vya wachezaji wapya kama ilivyo kuw akwa Tonado iliyopo sasa.

“Tonado ni moja ya  timu kubwa kwa Chake Chake na inayotoa upinzani mkali kwa vilabu mbali mbali, hata sisi Stone Town tunawaheshimu sana Tonado tunapokutana, tunajuwa tumekutana na timu kubwa na ngumu”alisema
.
Hata hivyo aliwataka walimu wa mskulini na Makocha wa mchezo huo, kuhakikiosha wanaibua vipaji vya wachezaji na kuwarithisha mikoba ya Tonado iliyokuwepo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.