Habari za Punde

Tanzeela Qambrani: Mwanamke mwenye asili ya Tanzania ateuliwa mbunge Pakistan na kuweka historia

Mwanamke mwenye asili ya Tanzania amekuwa wa kwanza wa asili ya Afrika kuteuliwa kuwa mbunge nchini Pakistan, na kutoa matumaini kwa watu wa jamii ndogo na maskini nchini humo yenye asili yake Afrika.
Tanzeela Qambrani, 39, aliteuliwa na chama cha Pakistan People's Party (PPP), cha waziri wa zamani Benazir Bhutto kuhudumu katika kiti kilichotengewa wanawake kwenye bunge la mkoa wa Sindh kusini mwa India.
Ana matumaini kuwa uteuzi wake baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita utasaidia kuondoa unyanyapaa ambao umekuwepo dhidi ya jamii ya Sidi, jina wanaloitwa watu wa asili ya Afrika wanaoishi maeneo ya pwani ya Makran na Sindh nchini Pakistan.
"Kama jamii ndogo iliyopotelea kwenye jamii kubwa za wenyeji, tumekuwa na wakati mgumu kudumisha mizizi yetu ya Afrika na tamaduni, lakini ningependa kuona kuwa jina Sidi linakuwa lenye heshima," Bi Qambrani ambaye mababu zake walitokea Tanzania aliiambia BBC.
Mwanamke huyo aliapishwa Jumatatu wiki hii na amenukiliwa na mtandao wa The News International akisema kwamba alijihisi kama Nelson Mandela.


Alivalia mavazi ya kitamaduni ya Kiafrika wakati wa kuapishwa kwake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.