Habari za Punde

ZRB yafika Tumbatu kuelimisha jamii umuhimu wa kulipa kodi

Na Hawa Ally, ZANZIBAR

KWAMARA YA KWANZA Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB imefika kutoa elimu ya mlipa Kodi katika kisiwa cha Tumbatu ikiwa ni muendelezo wa kuelimisha Jamii juu umuhimu wa kulipa Kodi kwa hiari. 

Elimu hiyo ambayao ilitolewa kwa wanafunzi wa skuli ya sekondari Tumbatu pamoja na baadhi ya walimu wa skuli hiyo. 

Akizungumza na wanafunzi hao Afisa Uhusiano wa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB Makame Khamis Moh'med alisema lengo la kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi ni kuwajengea uwelewa kufahamu juu maswala ya Kodi Ili na wao wawe walimu wa zuri kwa familia zao na hata katika maeneo yao wanayoshi. 

Katika elimu hiyo ambayo wanafunzi walipata kuelezwa mambo mbalimbali ikiwemo majukumu ya Bodi hiyo ya Mapato kama vile kuhamasisha ulipaji Kodi kwa hiari na kukuza ukusanyanyi wa Mapato kwa kutanua wigo wa Kodi. 

Aidha Afisa Uhusiano huyu alisema licha ya mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji Kodi katika vyanzo vyake vya Mapato lakini bado kunachangamoto ya kuwepo kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara bila ya kusajiliwa kulipa Kodi, biashara ya mafuta ya magendo nchini, wanunuzi kutokudai risiti. 

Kwa Upande wa mwalimu mkuu msaidizi wa skuli hiyo ya Tumbatu sekondari Makame Khamis aliipongeza Bodi hiyo ya Mapato kwa Mara ya Kwanza kufika kutoa elimu katika kisiwa hicho hususani kwa wanafunzi. 

Alisema wanafunzi ni walimu wa zuri katika kufikisha taarifa na anaamini elimu ya kulipa Kodi iliyotolewa na ZRB itawafikia Jamii husika katika kisiwa hicho. 

Hata hivyo nao wanafunzi wa skuli hiyo Mwanahawa Kombo alisema wamenufaika na elimu hiyo kwani hapo awali walikuwa hawafahamu majukumu ya ZRB licha ya kulisikia jina hilo masikioni mwao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.