Habari za Punde

TAKUKURU TANGA YAOKOA MILIONI 23 KWA KIPINDI CHA MIEZI MIWILI

 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga wakati akitoa taarifa ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Aprili hadi June 2019 kwa waandishi wa habari mkoani humo
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga wakati akitoa taarifa ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Aprili hadi June 2019 kwa waandishi wa habari mkoani humo
 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga wakati akitoa taarifa ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Aprili hadi June 2019 kwa waandishi wa habari mkoani humo
 AFISA Miradi wa Takukuru Mkoani Tanga Didas Mchau akitolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo kwenye kikao hicho kushoto ni Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali  wakichukua stori

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Tanga (Takukuru) imefanikiwa kudhibiti na kuokoa kiasi cha Sh.Milioni 23,009,860 kwa kipindi cha miezi miwili ambazo zimetokana na uchunguzi na wafanyabiashara “Wamachinga wa kigeni”

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Christopher Mariba wakati akitoa taarifa ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Aprili hadi June 2019 kwa waandishi wa habari mkoani humo

Alisema kwamba kati ya fedha hizo milioni 17.5 zinatokana na uchunguzi na milioni 5.5 zinatokana na wafanyabiashara “Wamachinga wa kigeni” waliobainika kufanya biashara katika Jiji la Tanga kinyume cha Sheria za Tanzania.

Mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Tanga alisema hilo linatokana na operesheni ya kushtukizwa kwa kushirikiana na vyombo vyengine vya dola na TRA mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu alfajiri katika makazi ya wageni ambao iliamini kwamba wamekuwa wakifanya lakini hawalipi kodi.

Aidha alisema katika operesheni hiyo taasisi hiyo ilikamata madaftari ambamo wahusika huandika kumbukumbu za mauzo yao na kuyakabidhi TRA ili waweze kukokotoa ukwepaji wa kodi unaofanywa na wageni hao.

Aliongeza kwamba Mamlaka ya Mapato TRA wamefanya kazi yao kwa mujibu wa sheria waliwafanyia makadirio kwa mwaka 2019 ambapo wamelipa kodi ya sh.milioni moja za kitanzania na faini ya milioni 4.5 kama adhabu kwa kukiuka sheria ya matumizi ya EFD.

“Vilevile wageni hao wameamua kuachana na biashara za ujanja ujanja,wamesajili biashara yao na kupewa TIN na kuanzia sasa watakuwa wanafanya biashara na serikali nayo kupata kodi yake” Alisema Mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Tanga.

Hata hivyo alisema kutokana na hali hiyo walitoa mapendekezo kwa ngazi za juu ili operesheni iliyofanyika Tanga iendeshwe kwa nchi nzima kuwabaini wageni wote wanaoshirikiana na wazawa kuhujumu uchumi wa nchi kwa kukwepa kulipa kodi huku wakijipatia fedha nyingi kwa kusingizio kwamba wanafanya utafiti wa soko kabla hawajaja kufungua biashara.

Wakati huo huo alisema kwamba katika kipindi hicho Taasisi hiyo imepokea jumla ya taarifa 70 za vitendo vya rushwa katika idara mbalimbali na uchunguzi wa taarifa hizo bado unaendelea kabla ya kufikia maamuzi mengineyo kwa kadri ya ushahidi utakaokuwa umapetikana.

Alisema kwa upande wa uendeshaji wa mashitaka mahakamani kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu Taasisi hiyo iliendesha jumla ya mashauri 25 ambapo mashauri 23 yalifunguliwa kabla ya Aprili 2019.

Hata hivyo alisema katika kipindi tajwa shauri namba (CC 45/2017) lilifika mwisho na kutolewa maamuzi ambapo mtuhumiwa alitiwa hatiani na kwenda Jela kutumikia kifungo cha miaka saba au kulipa faini ya milioni nne na mtuhumiwa huyo amekwisha tekeleza hukumu hiyo kwa kulipa faini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.