Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Awakabidhi Nishani Madaktari Bingwa wa Kichina Zanzibar Baada ya Kumaliza Muda Wao.

Na. Ali Issa Maelezo Zanzibar 10/72017
Waziri wa Afya Zanzibar Hamadi Rashidi Muhamed amewatunuku nishani madaktari wa kichina walio maliza muda wao wakutumikia kutoa huduma ya afya hapa Zanzibar katika matibabu mbalimbali yakiwemo mgonjwa ya upasuaji,koo na moyo.
Akitoa nishani hizo katika ukumbi wa dkt.Idrissa Adbuiwakili hapo kikwajuni Waziri hamadi alisema nishani hizo ni kutuwatunukia kutokana na kuweza kuitumikia Wizara ya Afya kwajuhudi zao za kitalamu kuwasaidia wananchi wa Zanzibar kuwapa matibabu bora.
Amesema Serikali ya Zanzibar imeridhika na huduma zao hivyo hakunabudi kuonesha utuwao kwa kuwapa nishani  hizo za upendo na utendaji bora kwa kazi walizo kuwa wakizifanya kilasiku.
Aidha waziri huyo alisema kuwa Serikali ya china na Zanzibar nimafrafiki wakweli wanao jaili haliza Zanzibar ndio maana kilamwaka wanakuja kutoa huduma za Afya Zanzibar tangu mwaka 1964 mara tu baada ya kuasisiwa Zanzibar.
Nae mkuu wa timu hiyo kwa niaba ya umoja wao wa madaktari hao wanao ondoka hapa Zanzibar kwenda kwao china dkt.Zhang Zhen alisema kuwa wamerizika na juhudi za Serikali ya Zanzibar na ukarimu na kuwajali na kukaa nao kama ndugu hali ambayo inaonesha wazi kuwa China na Zanzibr ni Marafiki wanao thaminiana na kujaliana utu kwa hali namali.
Hata hivyo alisema kuwa wao wanaondoka lakini tayari ipotimu mpya ya madaktari,anaamini kuwa watafanyakazi kwa ushirikiano kama walivyo kuwa wakifanyakazi wao.
Mkuu huyo aliomba ushirikianom kwa timu mpya ambayo ipo sasa ili iweze kuanyakazi kwa ufanisi zaidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.