Habari za Punde

Qwihaya Wamshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Magufuli Kwa Kuwapa Fursa Wamiliki wa Viwanda Wazalendo.

Mkurugenzi wa Qwihaya, Leonard Mahenda akisaidia wafanyakazi kutoboa nguzo za umeme 
Mkurugenzi wa Qwihaya, Leonard Mahenda akionyesha nguzo za umeme zilizotayari kwenda kutumika 

Na.Tumaini Godwin, Mafinga
Mafinga.  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya QWIHAYA GENERAL CO LTD inayozalisha nguzo za umeme mjini Mafinga, Mkoani Iringa Leonard Mahenda amemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapa fursa wamiliki wa viwanda  wazalendo kupata soko la uhakika ndani ya nchi.

Qwihaya ni kiwanda kilichoanza kuzalisha nguzo za umeme na kupata soko la uhakika ndani ya nchi baada ya Rais John Magufuli kuweka mkazo wa kutoagiza malighafi hizo nje ya nchi.

Akizungumza mjini Mafinga, Mahenda amesema kihalisia Tanzania ya viwanda imefungua fursa nyingi za kiuchumi ikiwamo kupanua wigo wa ajira.

 “Tanzania ya viwanda inanufaisha kuanzia makundi yote ya wakulima kwa sababu bidhaa na malighafi zinazozalishwa zinatoka ndani ya nchi,” amesema Mahenda.

Meneja Uzalishji  wa kiwanda hicho Fredy Gwega amesema kimefanikiwa kuajiri zaidi ya watanzania 300 wanaofanya kazi shambani, kiwandani na kwenye sekta ya  usafirishaji.

Kwa upande wake Mnunuzi wa nguzo za umeme na mkandarasi wa vifaa vya umeme Charles Mlawa wa Tropical anamshukuru Rais Magufuli na Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani kwa kufungua fursa kwa wazalishaji wa ndani.
“Tuna nguzo za kutosha kabisa na mimi mnunuzi napata bidhaa zinazotosheleza mahitaji, tunafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba hatuwaangushi viongozi wetu,” amesema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.