Habari za Punde

Skuli ya Sekondari ya Kangani Yakabidhi Cheti Cha Uhifadhi Mazingira Pemba


Mwanafunzi wa skuli ya Sekondari Kangani , Zulekha Silima , akimpatia Mkurugenzi  wa Baraza la Mji wa Mkoani Pemba, Rashid Abdalla Rashid,maelezo ya mti wa Muarubaini kama dawa asili , ikiwa ni baadhi ya miti inayopandwa na Wanafunzi hao katika mradi wa Eco-School, katika hafla ya makabidhiano ya cheti cha uhifadhi wa mazingira na Bendera ya Kijani ya Kimataifa  iliotolewa na mraddi huo kwa Skuli hiyo baada ya kufanya vyema katika uhifadhi wa mazingira.
Mkurugenzi wa Baraza la mji wa Mkoani Pemba, Rashid Abdalla Rashid , akipatiwa maelezo ya faida ya mti wa Mkarafuu kutoka kwa Mwanafunzi Fatma Muhamed Dadi,wa Skuli ya Sekondari ya Kangani katika Sherehe ya kukabidhiwa Bendera ya Kijani ya Kimataifa na Cheti ikiwa ni miongoni mwa Skuli zilizofanya vyema kwa Zanzibar kwa uhifadhi wa mazingira katika mradi wa Eco –School, iliofantika Skulini hapo.

Picha na Habiba Zarali  -PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.