Habari za Punde

Umakini na Uadilifu Miongoni mwa Viongozi Ndio Nguzo Pekee Itakayoimarisha Chama Katika Utekelezaji wa Katiba na Ilani Yake.

Mwenyekiti wa Jumuiya yua Wazazi Tanzania Mheshimiwa Edmund Bernad Mndolwa Kushoto akimueleza Balozi Seif  Mikakati ya Taasisi hiyo ya Chama katika muelekeo wake kwenye uchaguzi Mkuu ujao baadae Mwaka huu.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi kati kati akizungumza na Uongozi wa Juu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Tanzania uliofika Ofisini kwake kwenye Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Na.Othman Khamis.OMPR.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema uadilifu na umakini miongoni mwa Viongozi wanaosimamia Jumuiya za Chama ndio nguzo pekee itakayoendelea kuimarisha Chama Cha Mapinduzi katika utekelezaji wa Katiba na Ilani yake.
Alisema Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikipata Heshima kubwa na kuungwa mkono na Wananchi walio wengi Nchini kutokana na utekelezaji wa  Ilani na Sera zake kitendo kinachohamasisha hata Wanachama na Viongozi wa vyama vya Upinzani kuridhika na hatimae kujiunga na Chama hicho kikongwe Barani Afrika.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika Ofisi yake iliyomo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ilioongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Edmund Bernad Mndolwa.
Alisema changamoto zilizokuwa zikijichomoza ndani ya Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi ambazo ziliwahushisha baadhi ya Wanachama na hata Viongozi wake kwa sasa hazistahiki kupewa nafasi hasa ikizingatiwa kwamba Chama cha Mapinduzi katika miaka ya sasa kinaendeleshwa katika mfumo wa Kisayansi.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe wa Viongozi hao wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania kwamba Taasisi hiyo imebarikiwa kuwa na Rasilmali nyingi ikilinganishwa na Jumuiya nyengine za Chama Bahati ambayo lazima waizingatie na kuisimamia ipasavyo ili lile lengo la kuanzishwa kwake lifikie pazuri.
Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Mheshimiwa Edmund Bernad Mndolwa alisema Uongoziwa Taasisi hiyo ya Chama hivi sasa uko katika mchakato wa kuhakikisha CCM inaendelea kushika hatamu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae Mwaka huu.
Mheshimiwa Edmund alisema Viongozi wa Jumuiya hiyo wanaendelea na Mikakati ya muda mfupi na mrefu katika kuona malengo hayo yanatimia na kuleta mafanikio waliyoyalenga.
Naye kwa upane wa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Visiwani Zanzibar Nd. Haidar Haji Abdullah alisema suala la usafiri linapaswa kuangaliwa na kupewa msukumo mkubwa ili kuondoa changamoto inayowakabili Viongozi wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.