Habari za Punde

Waziri Mhe. Castico Akerwa na Watu Kugoma Kutowa Ushahidi Vitendo Vya Udhalilishaji.

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castrico akimkabidhi Cheti  Muandishi wa Habari wa Gazeti la Habari leo Ndg. Hatib Suleiman, baada ya kumaliza mafunzo ya  uandishi wa habari za mnaendeleo na uchuguzi wa udhalilishaji Wanawake na Watoto yalioandaliwa na  Jumuiya  ya  Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar  (WAHAMAZA)
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe.Mauldline Castico amesema matukio ya udhalilishaji wa kijinsia yamekuwa yakishamiri Zanzibar kwa sababu ya jamii kuoneana ''muhali'' na kukataa kutoa ushahidi Mahakamani.

Castico alisema hayo wakati akikabidhi tunzo kwa waandishi wa habari za maendeleo katika Jumuiya ya (WAHAMAZA) ambao walishiriki katika mradi wa kuandika habari za changamoto zinazowakabili wanawake na watoto katika kupata haki zao msingi.

Alisema wapo baadhi ya wananchi hawatowi ushirikiano katika kuzipatia ufumbuzi kesi za udhalilishaji wa kijinsia na matokeo yake ni kufutwa kwa kesi hizo Mahakamani.

''Tunazo sheria nzuri za haki ya watoto pamoja na kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia lakini tunakabiliwa na ''muhali'' ikiwemo kukataa kutoa ushahidi Mahakama''alisema.

Aliwataka waandishi wa habari kuendelea na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake na watoto ambazo ni kikwazo katika kuyafikiya maendeleo kwa makundi hayo ikiwemo sekta ya Elimu.

''Waandishi wa habari fanyeni kazi ya kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wanawake na watoto....tutatoa mashirikiano ya dhati katika suala hilo''alisema.

Katibu wa Jumuiya ya waandishi wa habari za maendeleo (WAHAMAZA) Salma Said alisema mafanikio makubwa yamepatikana katika mradi wa kuandika habari za maendeleo vijijini kwa ajili ya kufichuwa matukio ya udhalilishaji kwa watoto na kuona wanapata haki zao za msingi.

''Matatizo yanayowakabili watoto ni mengi ....juhudi zaidi zinahitajika kuona kwamba watoto wanaondokana na matatizo na changamoto ambazo ni kikwazo katika kuyafikiya malengo ikiwemo Elimu''alisema.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF)anayeshughulikia miradi Maha Damaj aliwataka waandishi wa habari kuendelea kutekeleza majukumu yao na kufanya uchunguzi wa matukio ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ambavyo hurudisha nyuma maendeleo ya watoto na ukuaji wao kwa ujumla.

''Bado hatujafanikiwa kukomesha vitendo vya udhalilishaji kwa watoto....nawaomba waandishi wa habari waliopata mafunzo hayo kuendelea kuzipatia changamoto zinazokwamisha watoto kupiga hatua kubwa ya maendeleo''alisema.

Jumla ya waandishi wa habari 15 walishiriki katika mradi wa  kuandika habari mbali mbali zinazohusu ukatili wa kijinsia kwa watoto ambapo miongoni mwa changamoto kubwa iliyobainika kwa watoto ni ukosefu wa vyeti vya kuzaliwa na kuwapa wakati mgumu wazazi wakati watoto wao wanapoanza Elimu ya msingi katika usajili wa kuanza shule.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.