Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein Ameongoza Kikao Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika viwanja vya Afisiu Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akiwasili katika viwanja vya Afisiu Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika viwanja vya Afisiu Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM  akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Bi. Laila Ngozi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na (kulia kwa Rais) Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi, wakiwa wamesimama baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, wakati wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua Kikaio cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.(kushoto kwa Rais) Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi. 



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.