Habari za Punde

Wanafunzi UDOM Wapagawisha Wananchi Katika Maonesho ya Nanenane Jijini Dodoma.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa kilele cha Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Kati yaliyofungwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stella Ikupa kwenye viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma. Walicheza ngoma moja yenye mchanganyiko wa ngomba za utamaduni za makabila mbalimbali nchini. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa (wa tatu kulia), Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Chemba ambaye pia ni Mwenyekiti wa wakuu wa wilaya za mikoa ya Singida na Dodoma, Simon Odunga pamoja na viongozi wengine wakifurahia ngoma iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakati wa kilele cha maonesho hayo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.