Habari za Punde

Wanahabari watakiwa kuelimisha jamii kujikinga na maradhi ya mripuko

Na Mwashungi Tahir           Maelezo    17-8-2020.
Waandishi wa habari wametakiwa kutumia vyema kalamu zao katika kuelimisha jamii juu ya kujikinga na maradhi ya mripuko ikiwemo corona na kuzingatia mazingatio yanayotolewa na Wizara ya Afya.
Ameyasema hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Wilaya ya Magharib A Ali amour Ali huko katika ukumbi wa Manispaa ulioko Kianga wakati alipokua akifungua mafunzo ya maradhi ya mripuko kwa wanachama wa ZPC kuhusu kuripoti habari za maradhi ya mripuko.
Amesema lengo la mafunzo haya kwa waandishi wa habari  ni kuhakikisha wanapata taaluma ili kuweza kufanya kazi kwa uadilifu na jamii iweze kupata uelewa na wajue vya kujikinga na maradhi hayo ya mripuko ambayo yametawala dunia nzima.
Hivyo amewaasa waandishi kutumia kalamu zao kwa kuwapa uelewa wananchi jinsi ya kutumia vigezo vilivyotolewa na Wizara ya Afya ili kuepukana na janga hili ambalo la kitaifa na  kimataifa
Pia amesema Ili yamalizike maradhi haya ni lazima wananchi tufuate maelekezo yanayotolewa na wataalamu tuweze kujikinga kwani madhara haya yakitukumba hakutokuwa na maendeleo nchini.
Hivyo tunawashukuru viongozi wa Serikali zote mbili kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt  Ali Mohamed Shein  kutoa kauli ya kuwashusha hofu wananchi  na kuwataka kuwa watulivu na kufuata mazingatio ya wataalamu.
Kwa upande wake mwandishi wa habari nguli Ali Sultani wakati akitoa mada ya muongozo wa namna ya kuripoti /kuandika habari ya maradhi ya mripuko amesema mwandishi wa habari ahakikishe anatoa ripoti zilizo sahihi ikiwemo kujua data zilizo sahihi.
Hata hivyo amesema waandishi wa habari kabla ya kuandika habari wafanye uchunguzi  kwa makini na ndipo wazitoe ili jamii iweze kufaidika na kuweza kujua maradhi ya corona yako vipi na tahadhari zake zichukuliwe kivipi ili wananchi waweze kuelewa.
Nao waandishi wa habari  wametoa michango yao kwa kutaka kuzingatia yale yote yanayotolewa na watu wa Wizara ya Afya na wameweza kufaidika kwa kujua vipi waripoti habari ikiwemo kujua mambo mengi yanayotakiwa kufanyika ili habari ziweze kutolewa kwa umakini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.