Habari za Punde

Breaking News Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemeid Suleiman Abdalla Ametangazwa leo Jijini Zanzibar .8/11/2020.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemeid Suleiman Abdalla emetangazwa leo   na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk. Hussein Ali Mwinyi. 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyiamemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilieleza kwamba  Rais Dk. Hussein Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 39 (1) na 39(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

 Kabla ya Uteuzi huo Hemed Suleiman Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.

 Uteuzi huo umeanza leo tarehe 08 Novemba, 2020.

 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.