RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar :-
1.Mheshimiwa Saada Mkuya Salum
2.Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita
3.Mheshimiwa Juma Ali Khatib
4.Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 07 Novemba 2020.
Aidha Viongozi hawa waliotajwa wanatakiwa waripoti Baraza la Wawakilishi Zanzibar kesho tarehe 08 Novemba, 2020 saa 6.00 mchana.
No comments:
Post a Comment