Habari za Punde

Rais Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi atembelea Kambi ya siku mbili ya utoaji wa huduma mbali mbali za macho kwa Wananchi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Pandu Ameir Kificho alipofika katika Skuli ya Sekondari ya Mpendae Wilaya Mjini katika kambi ya siku mbili ya utoaji wa huduma za macho kwa Wananchi zinazotolewa na Taasisi ya Beta Charitable Trust ya Uingereza.[Picha na Ikulu] 25/12/2020.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taasisi ya Beta Charitable Trust ya Uingereza Bw. Ayn Sharif,iliyoweka Kambi ya siku mbili ya utoaji wa  huduma mbali mbali za macho kwa Wananchi katika   Skuli ya Sekondari ya Mpendae Wilaya Mjini alipotembelea leo {Picha na Ikulu] 25/12/2020.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kiwana Mustafa  (katikati) alitembelea katika Madarasa mbali mbali ya Skuli ya Sekondari ya Mpendae Wilaya Mjini kuangalia Wananchi waliofika kuapata huduma ya macho inayotolewa na Taasisi ya Beta Charitable Trust ya Uingereza ambayo iliyoanza leo na itakuwa nia siku mbili na siku ya tatu  kuendelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.  [Picha na Ikulu] 25/12/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa nasaha zake kwa wananchi waliofika kupata huduma za afya ya macho leo  alitembelea katika  Skuli ya Sekondari ya Mpendae Wilaya Mjini  inayotolewa na Taasisi ya Beta Charitable Trust ya Uingereza ambayo iliyoanza leo  kwa siku mbili na siku ya tatu  kuendelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.  [Picha na Ikulu] 25/12/2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taasisi ya Beta Charitable Trust ya Uingereza Bw. Ayn Sharif (wa pili kushoto) wakati alipotembelea leo katika  Kambi ya siku mbili ya utoaji wa  huduma mbali mbali za macho kwa Wananchi iliyowekwa Skuli ya Sekondari ya Mpendae Wilaya Mjini   {Picha na Ikulu] 25/12/2020.
 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.