Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi afika Beit el Ajaib kushuhudia kuanguka kwa sehemu ya jengo hilo

Sehemu ya jengo la Beit Al Ajaib lilioanguka leo majira ya mchana 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo amali. Mhe Simai Mohammed Said wakati alipofika kujionea mwenyewe madhara ya kuanguka kwa jengo la Beit al Ajaib
Mkuu wa kikosi cha Zima Moto Zanzibar Ali Maalmus akifafanua jambo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi wakati alipofika kujionea mwenyewe madhara ya kuanguka kwa jengo la Beit al Ajaib
Gari la Ambulance likiwa eneo la tukio huku inasemekana kuna watu wane wamefukiwa na kifusi na jitihada za kuwaokoa zikiendelea
Wafanyakazi wa kikosi cha Zimamoto wakiwa katika eneo la tukio kujaribu kuwaokoa baadhi ya wafanyakazi ambao wanadhaniwa wamefukiwa na kifusi
Jeshi la Polisi  nalo wakiwa eneo la tukio kujaribu kusaidia kuweka utaratibu wa usalama kwa raia na eneo 
Wafanyakazi wa kikosi cha Zimamoto wakiwa katika eneo la tukio kujaribu kuwaokoa baadhi ya wafanyakazi ambao wanadhaniwa wamefukiwa na kifusi

Taarifa za karibuni ni kwamba watu wane wameokolewa na wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja kwa matibabu zaidi na hadi sasa hakuna aliyefariki.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.