Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi mgeni rasmi ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Kibuteni.

-Muenekano wa Skuli ya Sekondari kibuteni iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi na kupewa  jina la "HASNUU MAKAME" ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Vijana wa Mkoa wa Kusini Unguja wakisherehesha katika hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Kibuteni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Naibu katibu Mkuu CCM Zanzibar Juma Abdalla Mabodi katika hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Kibuteni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akifungua pazia kuangalia jiwe la ufunguzi la Skuli ya Kibuteni kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohammed Said.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi  (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari kibuteni kulia ni Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla kushoto ni  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohammed Said.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitembelea maeneo mbalimbali ndani ya Jengo jipya la  Skuli ya Sekondari Kibuteni.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi  akitembelea maeneo mbalimbali ndani ya Jengo jipya la  Skuli ya Sekondari Kibuteni.
Katibu Mkuu WEMA Dkt.Idrissa Muslih Hija akitoa maelezo ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa skuli ya Sekondari Kibuteni katika hafla ya Ufunguzi wa skuli hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohammed Said akizungumza machache na kumkaribisha Mgeni Rasmi kuhutubia katika hafla  Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Kibuteni.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katka hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Kibuteni.

 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi Rashid akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wananchi wa mkoa wake katika  hafla  Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Kibuteni.


PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.