Habari za Punde

Mashirikiano na Umoja wa Wamiliki wa Skuli Binafsi Yatasaidia Kuimarisha Sekgta ya Elimu Zanzibar. -Waziri Simai.

Na.Maulid Yussuf WEMA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Saidi amesema mashirikiano baina ya  Wizara yake na umoja wa wamiliki wa Skuli binafsi (ZAPS) yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya elimu nchini.

Amezungumza hayo wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya ziara ya jumuiya ya wamiliki wa Skuli binafsi ambayo ilifanya ziara katika Skuli hizo za Zanzibar,   katika ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Unguja.

Amesema  ili kuzitumia vyema fursa za elimu ni lazima kuwa na mashirikiano ya pamoja kwa kila mdau wa elimu ili lengo la kuzalisha wataalamu wazalendo lifikiwe.

Amesema moja kati ya matarajio ya Wizara ya Elimu Zanzibar na Jumuiya ya  Skuli binafsi ZAPS ni kutaka kulisukuma mbele gurudumu  la Elimu na kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu  hasa wa  daraja la kwanzafkl#u;wa wanafunzi.

Aidha Mhe Said amesema ni mpango wa Serikali ya awamu ya nane kuhakikisha kila kiongozi anakutana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuimarisha uchumi wa nchi.

Kwa upande wao Jumuiya ya wamiliki wa Skuli binafsi Zanzibar wamesema Zanzibar ina jumla ya skuli zaidi ya 50 za binafsi hivyo nazo zina nafasi kubwa ya kushirikiana na Serikali ili kuimarisha sekta hiyo.

Wamesema ufuatiliaji wa karibu  kwa Walimu na Wanafunzi pamoja na kuimarisha mazingira na upatikanaji wa vifaa utapelekea kupata matokeo mazuri zaidi kwa watoto.

Wamesema pamoja na mafanikio hayo lakini bado wanachangamoto mbalimbali ikiwemo kutoleshwa kodi na tozo kubwa ambazo hulipa Serikalini ambapo ameiomba Wizara kuwasaidia ili  waweze kupunguziwa ukubwa wa tozo na kodi ili waweze kuendesha shughuli zao vizuri.

Aidha wamesema Skuli binafsi zinaukosefu wa ruzuku kutoka Serikalini ambapo wameonba nao wapatiwe misaada ya vitabu na vifaa vyengine ili nao waweze kuendeleza vipaji wanavyozalisha kwanzia ngazi ya awali. 

Poa wameiomba Wizara ya Elimu Zanzibar kuwa karibu nao na kuwashirikisha katika masuala mbalimbali ya kuimarisha elimu nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.