Habari za Punde

Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) Kupaisha Elimu- Dkt.Ngumbi

Mkurugenzi wa TEWW  Dkt. Michael Ng'umbi akizungumza katika mkutano wa kujadili na kutoa maoni kuhusu Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) Ili kuboresha utekelezaji na uendeshaji wa programu za elimu ya watu wazima.

Mweshaji kutoka TEWW Bi. Leonia Kassamia akizungumza wakati wa mkutano kujadili na kutoa maoni kuhusu Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) Ili kuboresha utekelezaji na uendeshaji wa programu za elimu ya watu wazima.

Washiriki wa mkutano wa kujadili na kutoa maoni kuhusu Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) uliofanyika Mjini Morogoro Aprili 28 na 29, 2021 wakiwa katika mjadala wakati wa mkutano huo.

Washiriki wa mkutano wa kujadilina kutoa maoni kuhusu Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) Ili kuboresha utekelezaji na uendeshaji wa programu za elimu ya watu wazima. Mkutano huo uliofanyika Mjini Morogoro Aprili 28na29, 2021.



Na Mwandishi wetu- TEWW

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kushirikina na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na TAMISEMI imeandaa Mkakati wa Elimu Msingi na Mafunzo ya Watu Wazima (ABET) Ili kuboresha utekelezaji na uendeshaji wa programu za elimu ya watu wazima.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Michael Ng’umbi katika kikao kazi cha wadau kujadili na kutoa maoni kuhusu Mkakati huo kilichofanyika mjini Morogoro Aprili  28 na 29, 2021.


“Mkakati huu unatoa muongozi kwa wadau wa elimu nje ya mfumo rasmi kuhusu uendeshaji wa programu za elimu ya watu wazima, Commitment level, Financial support, Assessment system, Administrative structure na Innovation kwanzia ngazi ya wizara hadi serikali za mitaa,”alieleza Dkt. Ng’umbi


Akifafanua amesema, mkakati huo una himiza kutambua kwa wahitumi wa elimu nje ya mfumo rasmai kwa uwezo wao na kupewa fursa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo ya  taifa.


Wadau wa elimu nje ya mfumo rasmi walioshiriki katika kikao hicho ni wataalam wa elimu nje ya mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, TAMISEMI, UNESCO na maafisa Elimu ya watu wazima kutoka mikoa ya Mwanza, Tabora, Dodoma, Arusha, Singida na Mbeya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.