Habari za Punde

Uongozi wa Chuo Cha Zanzibar School of Health watoa Mkono wa Pole kwa Familia

Zanzibar School of Health (ZSH) inaungana na Wazanzibari na Watanzania wote katika mshtuko mkubwa uliolipata taifa kutokana na ajali ya basi huko Shinyanga na kuhusisha wanafunzi waliokuwa wakitoka masomoni huko Uganda. 

Chuo kinasikitika na kutoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao ambao ni Wahida Yussuf, Rehema Haji Juma na Nassor Juma.

Pia kwa huzuni kubwa tunawaombea wale wote waliopata majeraha makubwa na madogo. Lakini kubwa zaidi tunawaomba hilo lisiwe la kuwakatisha tamaa katika maisha maana vyovyote vile ni kadara ya Manani. 

Zanzibar School of Health inaguswa zaidi maana baadhi ya wanafunzi kwenye msafara huo waliofuata elimu ya juu huko Bugema University walipitia chuoni kwetu kwenye kiwango cha diploma. 

Zanzibar School of Health inaipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuchukua uamuzi wa kuwafuata wale waliofariki kwa njia ya haraka ya ndege na pia kusimamia mazishi yao. 

Na pia kuwa itasimamia matibabu ya majeruhi ambao bado wana nafasi ya kuwa nguvu kazi katika taifa. 

Kitendo hicho cha Serikali kitajenga uzalendo wa wananchi wetu na kinafaa kiendelezwe.

 *Uongozi ZSH*

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.