Habari za Punde

Zanzibar yaadhimisha siku ya wafamasia Duniani

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othman Simai akifungua Mkutano wa siku ya Wafamasia Duniani uliofanyika Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.
Prof. Raphael Zozimus Sangeda wa Muhimbili akiwasilisha mada ya elimu juu ya Virusi, chanjo na mabadiliko ya virusi kuhusiana na Uviko-19 wakati wa madhimisho ya siku ya wafamasia Duniani yaliyofanyika Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar.
Baadhi wa wafamasia wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa na watoa mada katika madhimisho ya siku ya wafamasia Duniani yaliyofanyia Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Utalii Maruhubi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafamasia Zanzibar Ame Omar Ame akichangia kuhusu kuongeza elimu wafamasia katika madhimisho ya siku ya wafamasia Duniani.
Mkuu wa ukaguzi wa dawa na utekelezaji (ZFDA) akiwasilisha mada yake ya kazi ya mamlaka za udhibiti katika ufuatiliaji wa chanjo za Uviko-19 katika maadhimisho ya siku ya Wafamasia Duniani.

 Picha ya pamoja ya baadhi ya wafamasia walioshiriki katika madhimisho ya siku ya wafamasia Duniani.

Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.