Habari za Punde

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS - SINGAPORE

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Novemba 14,2021 anatarajia kuondoka Nchini kuelekea Sentosa Island Nchini Singapore kushiriki mkutano wa  Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021 ) wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo muelekeo mpya wa kiuchumi baada ya athari za Uviko19.

Aidha Makamu wa Rais anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo  ya ana kwa ana na Viongozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wafanyabiashara pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo pamoja na Taasisi zao.

Mkutano huo unatarajia kufanyika kuanzia Novemba 16 hadi 19, 2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.