STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 27.01.2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi amemtakia kila la heri
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika siku
yake ya kuzaliwa hivi leo.
Katika salamu
hizo, Rais Dk. Mwinyi amemuombea kwa MwenyeziMungu Mama Samia Suluhu Hassan kuwa
na maisha marefu na yenye afya njema ili azidi kuendelea kuijenga Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania pamoja na watu wake wote, ambapo haya ni maadhimisho yake
ya kwanza ya siku ya kuzaliwa tokea ashike madaraka ya kuiongoza nchi.
Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,
Ikulu Zanzibar
No comments:
Post a Comment