Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango Azungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani Mei 23.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaofanyika Davos nchini Uswisi wakati wa mada ya ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa chakula duniani. Leo tarehe 23 Mei 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amesema katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa chakula duniani, nchi za bara la afrika zinaweza kufanya uwekezaji mkubwa katika kilimo na kuweza kutosheleza mahitaji ya chakula duniani.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani linalofanyika Davos nchini Uswisi alipochangia mada ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa chakula duniani. Amesema nchi za Afrika kutokana na kujaaliwa ardhi pamoja na maeneo ya uzalishalishaji katika sekta ya kilimo zinapaswa kuboresha sera ili ziwe rafiki katika kilimo ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa chakula.

Aidha Makamu wa Rais ameongeza kwamba nchi za Afrika zinapaswa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji na himilifu, kuwekeza katika miundombinu ikiwemo barabara  pamoja na kutenga ardhi kwaajili ya kilimo cha mashamba makubwa pamoja na wawekezaji. Ameongeza kwamba kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi kuna ulazima wa kuwekeza katika viwanda vitakavyozalisha pembejeo ikiwemo mboleo na mbegu.

Makamu wa Rais ameziasa taasisi za kimataifa za utafiti kuungana mkono jitihada za nchi za Afrika katika kuboresha afya ya udongo ili kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo. Aidha amesisitiza umuhimu wa suala la amani duniani ili kutoa fursa ya uzalishaji na usambazaji wa chakula duniani.,

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema Tanzania inapanga kutumia rasilimali watu hasa vijana katika mnyororo wa thamani wa kilimo kwa kutenga maeneo ya kilimo yatakayokwenda sambamba na huduma za pamoja kama vile huduma za ugani, pembejeo na masoko.

Mada hiyo imejadiliwa kutokana na dunia kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazopelekea upungufu wa chakula duniani kama vile Uviko19, vita pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Makamu wa Rais yupo Davos nchini Uswisi kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaoshirikisha wakuu wa nchi, wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa pamoja pamoja na wafanyabiashara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaofanyika Davos nchini Uswisi wakati wa mada ya ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa chakula duniani. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akishiriki katika ufunguzi wa mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaofanyika Davos nchini Uswisi Leo




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.